The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Mbunifu wa Nembo ya Taifa Afariki Dunia Muhimbili

0

Mzee Francis Maige Kanyasu almaarufu Ngosha, aliyekuwa akidai kwamba ni miongoni mwa watu waliobuni na kuchora nembo ya taifa, amefariki dunia usiku wa Mei 29, 2017 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo cha mawasiliano cha hospitali hiyo, iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaesha, Mzee Kanyasu alifariki dunia majira ya saa mbili na nusu usiku, baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Mzee Kanyasu alifikishwa hospitalini hapo Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokuwa akitibiwa, baada ya kituo kimoja cha runinga kumuibua akiwa anaishi maisha duni kwenye banda kuukuu maeneo ya Buguruni jijini hapa, ambapo baadaye ndipo serikali ilipoamua kumsaidia.

Akiwa hospitalini hapo, mzee Kanyasu alipata bahati ya kutembelewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli na mkewe, pia naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dk. Hamis Kigwangallah ambaye alikuwa mstari wa mbele kumsaidia.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

 

 

 

Leave A Reply