The House of Favourite Newspapers

Ndugu Waikataa Ndoa ya Mondi

0

OCTOBA 2, mwaka huu ambayo msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au Mondi alidaiwa kuwa angekuwa na jambo lake, ambapo ilikuwa siku yake ya kuzaliwa huku nyuma ya tukio hilo kumekuwa na madai kuwa, mzee baba huyo alitarajiwa kufunga ndoa ambayo ndugu wamekana kuifahamu.

 

MSIKIE NDUGU YAKE

“Mimi sina taarifa.” Alisema ndugu mmoja wa Mondi ambaye hakupenda kutajwa jina lake na kuongeza kuwa: “Hizo ni habari za mitandaoni na za vyombo vya habari, haiwezekani mimi nikawa sijui hadi leo Diamond anamuoa nani.

 

“Nisibishe sana huwenda ameamua kunifanyia suprise hata mimi, lakini mpaka sasa sijaona chochote kinachoashiria kuwa Diamond anaoa kesho.”Aliongeza kuwa, amekuwa akiona kwenye magazeti na vyombo vya habari taarifa za ndugu yake kuoa mwaka huu na mara kadhaa amekuwa akimuuliza Diamond na kukana.

 

MWINGINE ASEMA AKIOA AOE TU!

Wakati ndugu huyo akijibu hivyo, mwandishi wetu alazimika kumtafuta mmoja wa wanafamilia wa msanii huyo nyota Bongo mwenye hadhi ya “uzazi” na kumuuliza hizi taarifa za ndoa ya Mondi zimekaaje ambapo alisema:“We umesikia anaoa kesho?…sasa kama anaoa si mwache aoe kwani ubaya uko wapi?

 

“Ukiniuliza kuhusu maandalizi, mimi sijui chochote na wala sijui kesho kama kuna ndoa, kwa sababu sioi mimi anaoa Diamond, kama vipi muulize mwenyewe atakuambia kama anaoa au haoi.”

 

KWA DAMOND UKIMYA KAMA WOTE

Pamoja na kuwepo kwa tetesi za msanii huyo kuoa mwaka huu ambazo ziliwahi pia kupigiliwa msumari na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mondi mwenyewe amekuwa kimya kama vile anacheka kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari.Aidha, mameneja wa Mondi kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikataa kuelezea masuala ya uhusiano kuhusu msanii wao kwa madai kuwa, hayo ni mambo yake binafsi na siyo ya kikazi.

 

TANGAZO LA MONDI KUOA OKTOBA

Hakuna mwingine aliyekoleza taarifa za kufunga ndoa Oktoba 2, mwaka huu ni Diamond mwenyewe ambaye aliwaambia waandishi wa habari kwenye moja ya mikutano yake kuwa, Oktoba mbili atakuwa na jambo lake.“Sipo single nina mwanamke ninayetaka kuoa.

 

Sisi wengine sasa hivi hatutaki mahusiano, tunataka tuoe. Mwezi wa kumi tarehe mbili nitatimiza miaka 31 na sitaki kuwa tu na mwanamke, sitaki kuwa na kimada, sitaki kuwa na hawara, nataka kuoa,” alisema Diamond.Toka hapo, kilichokuwa kikitafutwa na media nyingi ni mwanamke gani anakuwa mke wa msanii huyo mkubwa Afrika?

 

Hapo ndipo pekuapekua zikajaa majina mengi ya warembo ambao wanahisiwa kupewa heshima ya kuitwa “mke wa Mondi” lakini bila mhusika kuthibitisha.Waliotajwa kupewa nafasi hiyo ni pamoja na mzazi mwenzake na msanii huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ raia wa Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, lakini akaenguliwa kiaina na wachunguzi wa mambo.Baada ya Zari kutupwa nje, nafasi yake alipewa Tanasha Donna raia wa Kenya na Hamisa Mobeto, wote hawa wamezaa na Mondi mtoto mmojammoja lakini pia karata ziligoma.

 

Aidha, katika hali ya kushtua akaibuka mwanadada Zuhura Othman ‘Zuchu’, ambaye ni memba mpya wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), inayomilikiwa na Mondi kuwa ndiye aliyetunukiwa nafasi ya kuwa mke wa Mondi.

 

Utamu wa habari hiyo umekuwa ukija na kukata kutokana na mapichapicha yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na kuwaacha njia panda wananchi wengi. Wasichana wengine waliotajwa kuwa na uwezekano wa kuolewa na Mondi ni Mbabazi Shadia ‘Shaddyboo’, mrembo kutoka Rwanda na mrembo mwingine kutoka Oman ambaye jina lake halijapatikana.

 

Hata, hivyo wadau wengine wa masuala ya kijamii wamemzungumzia Mondi kama ‘mzinguaji’, kwani mara kadhaa amekuwa akisikika kutangaza ndoa bila kutimiza ahadi yake.

Stori: Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply