The House of Favourite Newspapers

Paula Asisitiza: Simuachi Rayvanny

0

SIKU chache baada ya kuvuja kwa tetesi kwamba huwenda msanii wa Bongo Fleva, Rayvanny amerudiana na baby mama wake, Fahyma, mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Paula Kajala amesisitiza; “Simuachi Rayvanny…”

 

Madai ya Rayvanny kurejesha majeshi kwa Fahyma yaliambatanishwa na hoja kwamba wawili hao walionekana pamoja wakijivinjari kwenye mgahawa anaodai kuumiliki jamaa huyo uliopo Mbezi- Beach jijini Dar, wiki iliyopita.

 

Tetesi hizo ziliwashtua mashabiki ambao wana matumaini makubwa kwa kuwa penzi la Rayvanny na Paula siyo la kuvunjika leo wala kesho kwa namna wanavyopendana.

 

Sasa, wakati ishu hiyo ikiwa ‘hoti’, Paula amekanusha madai hao kwa kuposti picha ya Rayvanny akieleza kuvutiwa na macho yake ikiwa ni sehemu ya kuwajibu wakosoaji wake kwamba hatamuacha kwani anampeda.

 

Pia aliendelea kusema kwamba wakosoaji wake wanasumbuliwa na wivu. “Na simuachi nampenda. Wenye wivu endeleeni kupigwa shoti…” Aliandika Paula ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Uturuki huku Rayvanny akikatiza tu mitaa ya Bongo.

Leave A Reply