The House of Favourite Newspapers

Rais Zambia Afunga Mpaka Tanzania na Zambia – Video

0

RAIS Edgar Lungu wa Zambia ameamuru kufungwa kwa muda kwa mpaka nchi hiyo na Tanzania kuanzia  leo Mei 11, 2020.

Agizo hili limetolewa baada ya hivi karibuni kuthibitika kwa visa 76 vya #COVID19 katika Mji wa Nakonde unaopakana na Tanzania.

Visa hivyo 76 ni kati ya 170 vilivyotangazwa hivi karibuni na Waziri wa Afya nchini Zambia.  Jumla ya visa nchini humo ni 267, Vifo 7 na waliopona ni 11.

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave A Reply