The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Amlilia Mbunge Dkt. Kaburu

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa masikitizo kifo cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma, Dkt Walid Amani Kaburu kilichotokea usiku wa kuamkia leo Machi 7, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu

 

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu waCCM, Mkoa wa Kigoma, Dkt Walid Amani Kaburu kilichotokea usiku wa kuamkia leo Machi 7, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu..

 

“Dkt Walid Amani Kaburu atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki,” amesema Rais Dkt Magufuli katika salam zake za rambirambi zilizotolewa kwa umma na Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa.

Dkt. Amani Walid Kaburu aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.

Comments are closed.