The House of Favourite Newspapers

Ray, Mama Kanumba Kimenuka

0
Marehemu Steven Kanumba.

Na MWANDISHI WETU/GPL

DAR ES SALAAM: Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu bongo, marehemu  Steven Kanumba, Flora Mtegoa siku ya kumbukumbu ya mwanaye makaburini Kinondoni, alimfyatukia msanii wa filamu nchini,  Vincent Kigosi ‘ray’ aliyekuwa swahiba wa mwanaye kuwa, hajawahi kumuona hata siku moja makaburini hapo kuomboleza kifo cha mwanaye miaka yote ambayo hufanya kumbukumbu hiyo.

Vicent Kigosi ‘Ray” akiwa na mdau wa Filamu.

Akizungumza na Amani makaburini hapo, Aprili 7, mwaka huu,  mama Kanumba alisema kuwa, tangu aanze kuazimisha kumbukumbu za mwanaye hajawahi kumuona  Ray akiomboleza wala hata kuungana naye makaburini kama mastaa wengine wanavyofanya. “Yaani sijawahi kumuona huyo Ray akijumuika na sisi makaburini, utadhani yeye ataishi milele duniani.

Flora Mtegoa mama Kanumba. 

Kumbuka somo la leo kutoka kwenye Biblia linatufundisha kuwa, kila binadamu atakufa,” alisema mama Kanumba. Aidha, mama huyo alisema kuwa kama Ray na mwanaye waliwahi kuwa na ugomvi basi amsamehe kwani binadamu tumefunzwa kusamehe na sasa hayupo tena duniani.

“Unajua huenda walikoseana marehemu akiwa hai lakini mpaka leo naona kama ana kinyongo, asamehe tu. Naongea hayo kwa sababu sijawahi kuona akimuenzi hata kwa kufika makaburini kuungana na sisi, utadhani hakuwahi kuwa na uhusiano naye.

Nawashukuru sana wasanii wa kike wao ndiyo huungana na mimi katika maombolezo ingawa kwa mwaka huu hawakujitokeza lakini siwezi kuwasema vibaya kiukweli,” alisema mama huyo.

Baada ya habari hizi kutoka kwa mama Kanumba, Amani juzi lilizungumza na Ray aliyeamua kufunguka kuwa, yeye humuenzi Kanumba kwa njia nyingi tu si lazima kujionesha makaburini na si  lazima kuutangazia umma.

“Mimi najua marehemu alikuwa rafiki yangu na nimekuwa nikimkumbuka na kumuenzi kwa mambo mengi tu si lazima kuungana na mama Kanumba makaburini ndiyo nionekane,” alisema Ray kwa sauti yenye kumshangaa mama Kanumba kwa madai yake hayo.

 

Leave A Reply