Ray, Steve Nyerere pesa inaongea

ray nyerere na bella (1)
NA MUSA MATEJA

MASTAA wenye majina makubwa katika sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na rafiki yake Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, juzikati walithibitisha kuwa ‘pesa inaongea’ baada ya kuonekana wakimtunza ‘mpunga’ mrefu Christian Bella ambaye ni Kiongozi wa Kundi la Malaika Band katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

ray nyerere na bella (2)Katika usiku wa Novemba mosi mwaka huu ambako msanii nyota wa Nigeria, Wizkid alikuwa akifanya shoo, wawili hao ambao ni marafiki, waliwashangaza wapenzi wa muziki baada ya kushindana kummwagia pesa Bella wakati akiwajibika jukwaani.

Kabla ya kuanza kuoneshana umwamba huo, waigizaji hao walianza kutambiana kwa kila mmoja kujinadi kuwa ana uwezo wa kutunza kuliko mwenzake, ndipo muigizaji mchekeshaji, Steve Nyerere alipoanza kummwagia pesa Christian Bella ambaye wakati huo alikuwa anaimba moja kati ya vibao vyake vinavyotamba, Nashindwa.

ray nyerere na bella (3)Kuona hivyo, Ray naye akasogea mbele na kuanza kumtolea ‘wekundu wekundu’ Bella, kiasi ambacho kilionekana kuwa kikubwa kuliko cha Steve, kitendo kilichomrejesha tena kwa mara ya pili ili aweze kumpiku muigizaji huyo nyota wa filamu ya Kichwa cha Kuku.

Mchezo ukaanza kwa wawili hao kupokezana na kusababisha mashabiki waliokuwa karibu ‘kushadadia’ kwa kuwainua ili waendelee kummwagia fedha mwimbaji huyo na kwa hesabu za harakaharaka, kila mmoja alitoa kiasi kisichopungua shilingi milioni moja.

Mashabiki walioshuhudia kitendo hicho walipatwa na mshangao na kujiuliza ni wapi vijana hao wamepata fedha wanazoweza kuzimwaga kiasi hicho, huku wengine wakihusisha na kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, ambapo wawili hao walikuwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Duuh hawa jamaa, kama hizi fedha wanazoshindana kumtunza Bella ni za kampeni ya CCM, basi kweli watakuwa wamelipwa mshiko mrefu maana si mchezo wa kawaida huu, kwa pesa ilivyokuwa ngumu kipindi hiki unamuona mtu anamwaga pesa kama karatasi na hajutii, hii ni kali sana na jinsi wanavyoendelea hadi Bella anashuka jukwaani, hapa yawezekana wakawa wamefikisha milioni moja kila mtu,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, Steve Nyerere alikuwa miongoni mwa mastaa waliounda kundi lililopewa jina la Mama Ongea na Mwanao, lililozunguka na mgombea mwenza, Samia Hassan Sululu wakati Ray, yeye alikuwemo katika kundi lililopewa jina la Nimeshtuka, lililokuwa likifanya ziara ya kampeni katika mikoa mbalimbali Tanzania nzima.

Loading...

Toa comment