The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Staa Bongo Movie Afariki Dunia

0

TASNIA ya Filamu Tanzania ‘Bongo Movies‘ imepata pigo baada ya kuondokewa na msanii mwenzao, aitwaye Diana Choudry Nsumba ambaye amefariki dunia jana Jumanne, Desemba 31, 2019 baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani.

 

Akizungumzia msiba wa mwanaye, mama wa Diana amesema alifia njiani wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu. Msiba upo Magomeni Kagera karibu na Barabara ya Tandale kituo Popobawa.

 

Enzi za uhai wake, Diana aliwahi kufanya kazi na wasanii wengi lakini mara nyingi alifanya kazi zake na Muigizaji Rose Ndauka. Pia aliwahi kufanya kazi na Jimmy Mafufu.

Kwa mujibu wa taarifa ya mmoja wa wanafamilia, ibada ya kuaga mwili wa marehemu inafanyika sasa hivi na atazikwa leo Jumatano, Januari 1, 2020, majira ya saa 10 jioni katika makaburi ya Mburahati, jijini Dar es salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jimmy Mafufu ameandika;

Diana Choudry Nsumba mimi nilikuwa napenda kukuita Yezebeli kutokana na filamu tuliyowahi kuifanya pamoja zaidi ya miaka kumi iliyopita, ulikuwa binti wa kipekee sana mpole mwenye heshima na ulikuwa na nidhamu sana kazini.

 

Kusema za ukweli nimestuka sana baada ya kupata taarifa za kifo chako, Mungu pekee ndio anajua zaidi jinsi nilivyoumia.

 

Wewe ulikuwa rafiki yangu sana uliniheshimu mno hakika tasnia ya filamu imepoteza mtu muhimu lakini mimi nimepoteza dada na rafiki yangu wa moyoni ambaye hata tusipoonana mwaka lakini siku tukikutana tulikuwa kama tulikuwa wote jana tu.

 

Nenda dada yangu kipenzi nenda yezebeli mungu akuweke mahali unapostahili, na kama Mungu atayasikia maombi yangu hili nasema ni kama mungu atanisikia mjori wake basi ni maombi yangu yezebeli ulazwe mahali pema peponi uende mahali penye starehe ukapumzike paradiso kwa amani, rest in peace mylovely Yezebeli👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏

Leave A Reply