The House of Favourite Newspapers

VIDEO: OMMY DIMPOZ ALIVYOIBUKA KWA MHE JOKATE MLIMANI CITY


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz, anayetamba hivi Sasa na ngoma yake ya ‘Your The Best’ amejitokeza katika ukumbi wa Mlimani City kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tokomeza Zero iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo….

Kampeni ya ‘TOKOMEZA ZERO’ imelenga kuwasaidia wanafunzi waliopo katika shule za wilaya yake kupata mabweni na misaada mingine itakayowarahisishia na kuwajengea mazingira mazuri ya kusoma bila ya usumbufu.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ambaye ameongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jafo, ambao wote kwa pamoja wameunga mkono kampeni hiyo.

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar na kuhudhuriwa na Viongozi wa serikali, Wasanii wa muziki pamoja na waigizaji.

Comments are closed.