The House of Favourite Newspapers

Wangapi Wanataka Katiba Mpya?

0
 
DESEMBA 31, 2010 aliyekuwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza nia ya Serikali ya kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya. Pita huku nipite kule, mchakato wa kupata Katiba mpya ulitinga ndani ya Bunge Maalum ‘BMK’.
 
Wakati mambo yakikaribia kuiva, baadhi ya wajumbe na hasa kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi ‘Ukawa’ walijiengua kwenye ushiriki wa kupitisha Rasimu ya Pili ya Katiba hiyo na kuacha upande mwingine ukiongozwa na chama cha CCM kuendelea na mengine yaliyofuata na kutoka na kitu kinachoitwa Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa ikiwa tayari kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
 
Aprili 30, 2015 ilitangazwa kuwa siku ya wananchi kupiga kura zao za maoni, lakini jambo hilo liliyeyuka kiaina. Kelele zikabaki upande wa Ukawa “tunataka katiba mpya, tunataka katiba mpya.” Wenzao wa CCM wakabaki kimyaaa.
 
Hivi karibuni moto wa kudai katiba mpya ulianza kuwaka tena, wapinzani hasa wa Chadema wanasema hicho ndicho kipaumbele cha taifa kwa sasa. CCM kwa upande wao wanasema kipaumbele cha wananchi ni maendeleo yao siyo katiba.
 
Hebu tuwekane wazi hapa ni wangapi wanataka katiba mpya kwa sasa?
Na katiba hiyo ni ipi, ile ya Warioba au ile iliyochakatwa na Bunge la Katiba na mchakato uanzie wapi kufikia lengo hilo au tupotezee ishu hiyo, tupambane na hali ya maisha yetu tuone watoto wetu watapataje kipande cha muhogo?
 
@manyota_rich; 0714 895 555
Unaweza kutuma pia maoni yako.
Leave A Reply