The House of Favourite Newspapers

PAM D: Ningejichanganya, Unga Ungenichafua!

Pam D

Na ANDREW CARLOS|GAZETI LA IJUMAA|STAR MIX

WAKATI ishu ya madawa ya kulevya ikiendelea kuwa ‘hot’ kila kona ya nchi, staa wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amefungukia kuwa kipindi cha nyuma aliwahi kushawishiwa kujiingiza kwenye ishu hiyo kiasi kwamba kama angejichanganya, leo hii angechafuka vibaya.

Akizungumza na Ijumaa , Pam anayetikisa na Wimbo wa Popolipopo alisema, ishu hiyo ilitokea miaka ya nyuma wakati anaanza muziki ambapo alifuatwa na watu f’lani wakamshawishi ajiingize kwenye dili hizo akawachomolea akijua ni soo.

“Ujue nilikuwa natoka kimuziki na kipindi hicho kweli nilikuwa nimeanza kufahamika nchini pamoja na Kenya na Uganda. Sasa wakaja washkaji wakanishawishi niwe nafanya nao dili hizo. Niliwakatalia, sasa hebu fi kiria ningewakubalia kipindi hicho ingekuwaje kipindi hiki?” alihoji Pam D

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Comments are closed.