The House of Favourite Newspapers

UWT Wamtaka Ndugai Ajiuzulu

0

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi – CCM (UWT) Mkoa Arusha wamemtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ajiuzulu wadhifa wake huo ili awaachie watu wengine.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa Arusha, Yasmin Bachu leo, Januari 6, 2022 kufuatia kitendo cha Ndugai cha kupinga mkopo wa shilingi Trilioni 1.3 uliokopwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

“Tumechoka kuvumilia tabia za Ndugai za udhalilishaji kwa Kiti cha Urais kitokanacho na CCM, tunamtaka atuachie Kadi yetu ya CCM na Pili ajiuzulu Nafasi yake ya Uspika haraka kabla hatujachukua Hatua Stahiki Dhidi yake.

 

“Tunampongeza Mhe. Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama yetu na Jemedari wetu Mkuu Samia Suluhu Hassan kwa kazi Nzuri anazozifanya za Kupigania Maendeleo ya Nchi yetu pasipo Kuchoka na kwa Juhudi Kubwa.

 

“Kiongozi ambaye yupo hapo alipo kwa tiketi na hisani ya Chama cha Mapinduzi ikiwa hawezi kumheshimu tena Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wetu, basi atumie Busara ndogo iliyobaki kujiuzulu ili kulinda hata hiyo heshima ndogo kabisa aliyobaki nayo,” amesema Bachu.

Leave A Reply