The House of Favourite Newspapers

Wanne Yanga Waipoteza Simba Yote

STORI:  Ibrahim Mussa| CHAMPIONI | Dar es Salaam

MABAO yaliyofungwa na wachezaji wanne wa Yanga, Simon Msuva, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Obrey Chirwa katika Ligi Kuu Bara msimu huu, yameonekana kuwa ni mengi kuliko yale yote yaliyofungwa na Simba.

Yanga ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 49, jumla imefunga mabao 46 msimu huu, huku wachezaji wake hao wanne wakifunga mabao 35.

Ngoma

MAKwa upande wa Simba ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 48, yenyewe imefunga jumla ya mabao 33 ambayo ni pungufu ya mawili kuyafikia yale yaliyofungwa na nyota hao wanne wa Yanga.

Msuva ambaye ni kinara wa kuzifumania nyavu mpaka sasa katika ligi hiyo, amefunga mabao kumi, Tambwe amepachika mabao tisa, Ngoma na Chirwa kila mmoja amefunga mabao nane.

Tambwe.

Kwa maana hiyo, safu ya ushambuliaji ya Yanga ni imara zaidi kuliko kikosi kizima cha Simba ambacho kwa zaidi ya misimu minne sasa hakijafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara tangu mara ya mwisho walivyouchukua mwaka 2012.

Chirwa

Hii inaonyesha kuwa kama Yanga wakiendelea kufunga mabao mengi namna hiyo, watakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

TAZAMA VIDEO MAGUFULI ALIVYOPIGILIA MSUMALI SKATA LA MADAWA

Save

Comments are closed.