The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Madawa ya Kulevya Imezima Ngoma Hizi…

Daimond Platnumz

Na ANDREW CARLOS| IJUMAA WIKIENDA| OVER ZE WEEKEND

ZIMESHAPITA wiki mbili sasa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza vita dhidi ya watumiaji na wahusika wa madawa ya kulevya huku akitaja majina ya wanaotuhumiwa wakiwemo viongozi wa kidini, kiserikali, wasanii na polisi.

Lakini tangu kuwepo kwa ishu hiyo ambayo imehusisha mastaa wengi kwenye tasnia ya muziki na filamu wakiwemo TID, Wema Sepetu, Petit Man, Recho,Tunda na Lulu Diva (wapo nje kwa dhamana), macho na masikio mengi ya mashabiki kwenye redio, TV na mitandao mbalimbali ya kijamii nchini yamekuwa katika kufuatilia ishu ya madawa jinsi inavyoendelea ambapo kila siku mapya uibuka na kusahau baadhi ya vitu vingine ikiwemo muziki.

Ikumbukwe kuwa, katika kipindi hiki wapo wanamuziki wakali ambao wameachia ngoma zao lakini zimeonekana kufunikwa na ishu ya madawa ya kulevya na huenda mpaka ishu hii itakapofifia ngoma zao zinaweza kuonekana za kawaida. Katika makala haya, nakuchambulia baadhi tu ya ngoma hizo ambazo zimefunikwa na ishu hiyo;

DIAMOND FT NE-YO – MARRY YOU

Daimond Platnumz (Kushoto) na Neyo

Mashabiki walianza kuipenda ngoma hii mwaka jana ilipovuja kipande cha video. Wengi walikuwa wakiisubiri kwa hamu kuiona yote sambamba na kuisikia kwa sababu ilikuwa ni kolabo ya kwanza aliyoifanya Diamond na staa kutoka nchini Marekani. Ngoma hii ilianza kuachiwa kimataifa na kampuni kubwa ya muziki ya Universal Music Africa kisha nchini Tanzania. Licha ya kupewa promo za kutosha na interview, bado mashabiki hawajaiwekea masikio yote kutokana mitandao ‘kuchafukia’ ishu ya madawa.

LINEX – KIHEREHERE

Linex

Kwa muda mrefu Linex alikuwa amepotea kwenye gemu ya Bongo Fleva. Mara ya mwisho kuibuka na ngoma kali ilikuwa mwanzoni mwa mwaka jana akiwa na Ngoma ya Kwa Hela. Kwa mwaka huu, Linex amejipanga kuuanza mwaka vizuri baada ya kuachia Ngoma ya Kiherehere lakini kutokana na ishu hii ya madawa, ngoma hiyo kali kidizaini kama imegoma kusogea na kuwafikia mashabiki wengi.

JOH MAKINI – WAYA

Joh Makini

Mwaka juzi kuingia mwaka jana alifunga na kufungua mwaka vilivyo na Ngoma ya Don’t Bother aliyomshirikisha staa kutoka Sauz, AKA. Ilikuwa kolabo yake ya kwanza kimataifa na mwaka jana katikati akadhihirisha kuwa ni wa kimataifa zaidi baada ya kuibuka tena na Ngoma ya Perfect Combo akiwa amemshirikisha staa kutoka Nigeria, Chidinma. Mwaka huu amefungua na Ngoma ya Waya, ni ngoma kali kuisikiliza hata kuicheza lakini licha ya kufanya interview na promo za kutosha nchini, mapokeo yake yanaonekana kufifia kutokana na uwepo wa ishu hii.

CHEGGE – KELELE ZA CHURA

Chegge na Nandy

 

Kama ilivyo kwa Joh na Linex, Chegge naye ni miongoni mwa wakali waliosumbua mwaka jana baada ya kuibuka na Ngoma ya Waache Waoane akiwa amemshirikisha Diamond Platnumz. Mwaka huu ameamua kufanya kitu cha tofauti ambapo ngoma yake mpya ya Kelele za Chura amemshirikisha msanii wa kike anayekuja kwa kasi kutoka THT, Nandy.

Licha ya kuifanyia promo za kutosha, bado ngoma hiyo haijakaa vizuri kutokana na ishu ya madawa. Bill Nass , Country Boy,Stereo,Young Killer,Adam Mchomvu,Stamina,Nyandu Tozz – MAN 2 MAN Mashabiki wengi hususan wa Hip Hop Bongo watakuwa bado hawajaisikia ngoma hii kutokana na kufunikwa na ishu ya madawa ya kulevya.

Man 2 Man ni moja ya kolabo kali zilizoshirikisha wakali wengi wa Hip Hop kwa pamoja ikiwa na michano ya kutosha.

RAY C – UPEPO COVER

Ray C

Kwa kipindi kirefu inajulikana kama Ray C ‘Kiuno Bila Mfupa’ alikuwa kimya kimuziki kutokana na kuwepo kwenye tiba ya kujiondoa na matumizi ya madawa ya kulevya. Mwaka huu ameachia ‘bonus track’ ambayo ni ‘cover’ ya Upepo iliyowahi kuimbwa na Recho wa THT huku lengo lake likiwa ni kuwaweka sawa mashabiki wake kabla hajaachia ngoma yake mpya. Lakini hadi sasa si mitandaoni wala redioni, ngoma hii haijapata shavu zaidi ya ishu ya madawa kuendelea kutikisa.

Christian Bella

FT. KHALIGRAPH – OLLAH

Wengi walipoambiwa ujio wa kolabo hii ya King of the Best Melodies kutoka Bongo, Christian Bella na mkali wa Hip Hop kutoka Kenya, Khaligraph Jones walikuwa na shauku kubwa ya kuisikia. Bella alifanikisha yote hayo lakini kitendo cha kuiachia katika kipindi hiki ambacho mashabiki wengi wa muziki wakiweka masikio yao na macho kwenye ishu ya madawa, ikasababisha ngoma hii kuwafikia mashabiki wachache.

Comments are closed.