The House of Favourite Newspapers

Jimmy Mafufu Ataka Mabachela Wapimwe Akili!

0
Jimmy Mafufu wa kwanza kulia akiwa na wasanii wengine wa Bongo Muvi.

Na GLADNESS MALLYA| RISASI MCHANGANYIKO| ZA MOTOMOTO

MSANII wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu amewatolea uvivu waigizaji ambao umri wa kuoa au kuolewa umefi ka, lakini kwa kuendekeza starehe wameshindwa kufanya hivyo, akitaka wapimwe akili kwa vile anaamini hawako sawa.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Mafufu ambaye ni mmoja wa mastaa wanaofanya vizuri katika ‘game’, alisema wasanii wengi waliowahi kuigiza wanaoa au kuolewa kwenye fi lamu ambao umri wa kuoa au hawajaingia kwenye ndoa, hivyo wanapaswa kumuomba Mungu awasaidie waache kuendekeza starehe.

“Mtu asiyetaka kuoa au kuolewa anatakiwa apimwe akili au apewe ushauri nasaha, ikishindikana afanyiwe dua au maombi maalum maana ustaa siyo kigezo cha kubadili wapenzi, jambo ambalo linaleta picha mbaya kwa jamii, nawasihi wasanii tujitambue na tuache kuendekeza starehe,” alisema Mafufu.

 

Leave A Reply