Hamorapa, Ney Wamitego lao Moja

Hamorapa na mpenzi wake.

Stori: Na Andrew Carlos | IJUMAA | SHOWBIZ

KIZUNGUMZIA ishu ‘inayo-trend’ kwa sasa kwenye burudani hususan katika Muziki wa Bongo Fleva bila kupapasa utataja ishu ya msanii chipukizi aliyejizolea umaarufu wa ghafla, Athuman Omary ‘Harmorapa’.

Harmorapa amejizolea umaarufu kutokana na kuhusishwa kufanana muonekano na staa wa muziki huo ambaye ni mmoja kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’. Licha ya kuhusishwa huko, pia jina lake lina ukaribu na Harmonize ila utofauti wa hao wawili, Harmorapa anafanya Muziki wa Hip Hop wakati mwenzake anaimba.

  Kimuziki

Harmorapa amefahamika wiki tatu zilizopita kupitia ngoma yake ya Usigawe Pasi ambapo katika video ya ngoma hiyo amemtumia dada anayefananishwa kimuonekano na muigizaji kutoka Bongo Muvi, Jacqueline Wolper. Ikumbukwe kuwa Wolper yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Harmonize.

Tangu kufahamika kwa dogo huyo ambaye anatokea mkoani Mtwara kama ilivyo kwa Harmonize, mashabiki wengi wa muziki wamekuwa wakimuongelea na wengine kumfuatilia kwa ukaribu.

Kushika mkwanja

Hamorapa

Moja ya matukio ambayo yamewashtua wengi ni kitendo cha kuonekana na ‘maburungutu’ ya pesa ‘mkwanja’ jambo ambalo limewahi kufanywa na wanamuziki wengine hivi karibuni kama vile Nay wa Mitego na Rayvanny.

 

Nay akitamba na mkwanja.

Itakumbukwa kuwa, baada ya picha za Nay akiwa amekumbatia maburungutu ya pesa kusambaa mitandaoni, alifanyiwa mahojiano katika kipindi kimoja cha TV, juu ya utajiri wake huo na kusema kuwa biashara pamoja na muziki wake ni vitu vinavyomwingizia pesa nyingi.

Ney wa Mitego na Mpenzi wake

Alisema mali zake na kila kitu zinafika bilioni, ukichanganya hela zilizo benki pamoja na biashara anazofanya thamani yake.

Kwa upande wa Harmorapa kwake ameonesha kumbe inawezekana kushika pesa hizo ndani ya muda mfupi. Hivi karibuni naye aliachia picha kibao zikimuonesha akiwa na maburungutu ya pesa.

Swali ni je, pesa hizo ni zake alizozipata ndani ya kipindi kifupi tangu aingie kwenye muziki au kachukua tu ili apigie picha na kutafuta kiki? Kama kafanya kwa lengo la kiki, tuna-wezaje kuamini kwamba zile walizopigia picha akina Nay wa Mitego  ni zao? Jibu utakuwa nalo wewe msomaji?

Kumiliki gari

Licha ya kuonesha mkwanja huo, Harmorapa pia anadaiwa kuzawadiwa mkoko aina ya Nissan Murano na meneja wake ambapo jambo kama hilo limeshawahi kutokea kwa wasanii wengi wa muziki wa Bongo Fleva kukabidhiwa mkoko na mameneja wao kama vile Rayvanny, Queen Darleen na Dogo Janja.

Katika hili nalo bado kuna siri nyuma ya pazia! Hivi kweli gari hilo kapewa au nalo kaomba apigie picha? Maana alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha TV hivi karibuni, dogo huyo alionekana kutuna kabisa kwenye usukani wa gari hilo kuonesha ni lake lakini baadaye kuna picha kapiga yuko kwenye siti ya abiria.

Nay na Siwema.

Kubadili wanawake

Alipoanza kuonekana kwenye video alikuwa na Wolper Feki na hata katika ‘interview’ mbalimbali za TV na redio alizokuwa akifanyiwa alikuwa akiongozana na Wolper huyo.

Lakini kwa siku za hivi karibuni alimtambulisha mwanamke mwingine kuwa ndiye aliyenaye baada ya kumpiga chini Wolper Feki. Mwanamke wake mpya ni video queen ambaye yupo katika Video ya Too Much ya Darassa.

Harmorapana Wolper Feki

Kwa anachokifanya Harmorapa ndani ya muda mfupi kubadili wanawake, ni jambo ambalo wasanii wengi nao wamekuwa wakifanya hivi katika uhusiano wao akiwemo Nay ambaye alishawahi kutoka na Shamsa Ford, Siwema na pia akadaiwa kutoka na Pam D.

Ndiyo maana naweza kusema kuwa, anachokifanya Harmorapa ndicho wanachokifanya wasanii walio wengi na kwa hili niseme tu kwamba ni ulimbukeni!

Video: Harmorapa Kaitoa Wapi Jeuri Hii?

Save

Toa comment