
Browsing Category
Makala
Kama Haoni Umuhimu Wako, Muombee Aishi Miaka Mingi!
JUMATANO nyingine Mungu ametukutanisha. Kama ilivyo kawaida, hapa huwa tunajadili mambo mbalimbali yahusuyo masuala ya mahusiano. Ili uweze kuishi vizuri, binadamu unahitaji mahusiano mazuri na binadamu wenzako. Iwe ni rafiki wa…
Faida, Hasara Za Wapendanao Kuambizana Ukweli!
UKIZUNGUMZA na wanaume wengi kwa sasa, watakuambia wanawake siyo wa kuwaeleza kila kitu katika uhalisia wake. Wanatakiwa kudanganywa kidogo ili mambo yaende. Wanaitumia hiyo kama silaha wakidai kwamba wanawake ni watu ambao wakijua kila…
Madhara ya mke kuwa muongeaji kupitiliza Yapa Hapa
USHAWAHI kukutana na mwanamke anaongea sana? Yaani yeye ni bandika bandua. Likiisha hili anaingiza hili, anajua kila kitu. Ana ujasiri wa kuzungumza kwelikweli hata kama waliomzunguka wote ni wanaume. Akianza kuongea jambo lake…
Mfanyie Haya Mpenzi Wako Penzi Lidumu
KATIKA mapenzi kuna vitu vingi unaweza kumfanyia mpenzi wako ukamfurahisha na kumfanya azidishe mapenzi kwako. Katika safu hii leo nitazungumzia mambo machache muhimu yatakayokusaidia kuboresha nakudumisha penzi lako kwa umpendaye.…
Achana Na ‘Siwezi Kuishi Bila Yeye’, Kuna Maisha Bila Yeye!
HAKUNA shaka tulio wengi tupo katika uhusiano wa kimapenzi wa mashaka. Hakuna hata mmoja wetu ambaye anaweza kujiaminisha kwa asilimia mia moja kwamba mpenzi wake aliye naye anampenda kwa dhati kabisa au anazuga. Hii inabaki kuwa siri…
Makosa Yanayosababisha Wanawake Wasiolewe Yapo Hapa!
WAHENGA huwa wana misemo yao ile kwamba sijui kuolewa ni bahati, kuolewa ni tabia na mingine mingi tu. Leo nataka tujadili juu ya makosa ambayo wanawake wengi wanayafanya na kujikuta wakishindwa kuolewa. Wanawake wengi wamekuwa…
Kauli Wanazopenda Wanaume Kuzisikia Kwa Wenza Wao, Zipo Hapa
HAKUNA kitu kizuri kwenye uhusiano kama kujua mwenzako anapenda nini. Unapomjua mwenzako anachokipenda, itakusaidia katika suala zima la kudumisha uhusiano. Ukimfanyia yale anayoyapenda, sio kwamba atafurahi tu bali unamtengenezea…
Unaweza Kupata Mwenza Sahihi Mitandaoni?
DUNIA ya sasa mambo yamekuwa rahisi. Teknolojia imefanya vitu vingi ambavyo vilikuwa vinachukua mlolongo mrefu kutendeka kwa muda mfupi tu. Waswahili wanasema ni kama vile kumsukuma mlevi jinsi ambavyo mambo yamekuwa rahisi.
Kama…
Namna Ya Kuishi Na Mpenzi Mwenye Mawazo Hasi, Soma Hapa
MTU mwenye mawazo, ni yule ambaye muda wote anayatazama mambo kwa ubaya, analalamika, analaumu wengine, anapenda kuwashambulia wengine kwa kauli za kuudhi na zisizo za kiungwana na muda wote anaamini kwamba yeye hakosei.
Mtu wa namna…
Jinsi Ya Kukwepa Kurubuniwa na Kumsaliti Mpenzi Wako.. Wanaume/Wanawake Soma Hapa
WAPO watu ambao wameoa au wana wapenzi walioahidiana kwa mambo mengi, lakini wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kuvutwa kimahaba na watu wengine. Hali hii huwatokea wawapo masomoni, kazini, kwenye biashara, mbali au pengine hata karibu na…
Mbinu za Kumfanya Aamini Kama Kweli Unampenda kwa Vitendo
NENO ‘nakupenda’ ni dogo lakini lina maana kubwa sana kwa anayelitamka na anayetamkiwa. Kwa bahati mbaya sana, siku hizi neno hilo limekuwa kama mzaha, kila mtu analitamka, wakati mwingine hata mahali pasipostahili na wakati mwingine…
Kwa nini wachumba wanakupiga kibuti kila mara? Soma Hapa
UHUSIANO wa kimapenzi kwa vijana wengi hukumbwa na changamoto nyingi. Zipo sababu kadhaa zinazosababisha hilo, lakini kubwa zaidi ni ugeni wa mambo ya mapenzi na kutokupata elimu sahihi juu ya maisha ya urafiki na uchumba kabla ya ndoa.…
Mbinu Sahihi za Kumaliza Stress za Mapenzi, Soma Hapa
SIKITIKO la mahaba lashinda msiba! Umewahi kusikia maneno hayo ya wahenga? Bora usimuliwe lakini usipitie kipindi cha sikitiko la mahaba. Hakuna kipindi ambacho unaweza kuhisi kama dunia imefika mwisho kama pale unapoumizwa na yule…
Mwenzi Wako Akikuonyesha Haya, Jua Hakutaki!
KWA kawaida mtu anapompenda mtu huwa ni vigumu sana kumuacha aende. Hatamani hata siku moja kumpoteza mtu ampendaye. Atafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba mhusika anakuwa mpenzi wake.
Mapenzi humfanya mtu awe kipofu.…
Jinsi Ya Kuepuka Kupotezewa Muda Kwenye Mapenzi
RAHA ya uhusiano wa mapenzi ni kumpata mwenza sahihi na kwa wakati muafaka. Unapopishana na muda, unachelewesha maendeleo yako maana mapenzi ni chachu ya maendeleo. Ili uingie kwenye familia, inakupasa uingie katika muda sahihi na mtu…
Uvumilivu Una Kikomo, Hata Kama Ni Mzuri Vipi Bora Umuache!
KUNA huu msemo usemao, mvumilivu hula mbivu. Hakuna ambaye ni mgeni wa msemo huu, hukuna asiyejua elimu tunayoipata kutokana na msemo huu. Hakika siku zote mvumilivu mwishowe hula mbivu licha ya kwamba inatahadharishwa kuwa makini sana…
Hizi Hapa Faida saba za Tango Mwilini Mwako
HAWANA makosa wale waliosema kuwa mboga za majani na matunda ni kinga kwa afya yako. Matunda mengi yana manufaa lakini tango linaonekana kutia for a kwa manufaa katika mwili wa binadamu. Tango ni aina ya tunda jamii ya tikitimaji kwani…
Marafiki, Wanajenga, Wanabomoa Uhusiano, Jifunze!
DUNIANI tunaishi kwa kutegemeana. Kwenye maisha kila mtu anamhitaji mwenzake kwa namna moja au nyingine. Anahitaji msaada wa mawazo, ushauri na hata fedha hivyo mtu huwezi kuepuka marafiki. Marafiki ndio ambao wanaweza kukupa msaada…
Madhara Ya Kumchunga Mpenzi Wako Bila Sababu!
MPENZI msomaji wangu, kilio cha wengi walio kwenye uhusiano ni kuhisi wanasalitiwa na wapenzi wao waliotokea kuwaamini sana. Wapo ambao si tu kwamba wanahisi bali wanawafumania kila kukicha wapenzi wao licha ya imani…
Silaha 5 za Mwanamke Kumteka Mwanaume Kimapenzi
KATIKA maisha ya mapenzi watu wanapaswa kuelewana na kusikilizana mno. Hii ndiyo silaha kubwa zaidi kuliko zote na rahisi zaidi ya kukaa pamoja kwa muda mrefu. Pia mkisikilizana itasaidia wawili mnaopenda kudumu kwenye ndoa u uhusiano wenu…
Mambo 5 Unayotakiwa Kujua Kuhusiana Na Hedhi
NI vema kujua haya tutakayoyaainisha hapa leo. Inakadiriwa kuwa, mwanamke hupata hedhi wastani wa mara 400 katika maisha yake.
Pia, neno linalotumika sana kuwakilisha hedhi ni ‘period’, lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye…
Madhara ya Wapenzi Kugombana na Kununiana Mara kwa Mara
MWISHONI mwa wiki iliyopita, nilipata bahati ya kukutana na mmoja kati ya wasomaji wangu wa siku nyingi ambaye amekuwa akiufuatilia ukurasa huu na kujifunza mambo mbalimbali.
Alikuwa na shida iliyomfanya anitafute na alichonieleza,…
Kama Anakuliza Kila Siku, Unamng’ang’ania Wa Nini?, Soma Hapa
TUNAPOKUTANA kama hivi, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani wapo ambao muda huu wako kitandani wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali huku wengine wakiwa wameshatangulia mbele za haki.
Ndugu zangu, mapenzi yamekuwa yakiwaliza…
Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa Kwanza Katika Historia
Miss Tanzania wa kwanza, Theresa Shayo akipita kwenye kingo za bwawa la kuogelea la hoteli ya Kilimanjaro mwaka 1967.
Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika…
Ukitaka Penzi Lako Lidumu, Fanaya Haya Tangu Mwanzo!
HAKUNA muda ambao hisia za mapenzi na msisimko huwa mkubwa kama kipindi ambacho ndiyo kwanza mnaanzana. Ukiwauliza watu wengi leo ambao wanateswa na mapenzi, wanatamani siku zirudi nyuma ili warudie kufaidi mapenzi kama ilivyokuwa siku…
Hata Kama Upo Naeye Kwenye Ndoa, Unapaswa Kumpa Uhuru Wake
HATA Jinsi tulivyoumbwa, kila mmoja anapenda sana kuwa na ule uhuru wake wa faragha au kwa Kingereza wanaita privacy. Huu ni muda ambao mtu anakuwa peke yake na kufanya mambo yake peke yake bila kuingiliwa na mtu yeyote. …
Kuna Maisha Baada Ya Kutendwa Soma Hapa Ujinasue!
MARA nyingi inapotokea umejeruhiwa penzini hususan kwa mtu ambaye ulikuwa na malengo naye ni vigumu sana kupenda tena.
Ni vigumu sana kumuamini tena mtu wa jinsia tofauti na yako. Wakati mwingine unaamini mtu wa jinsia ya tofauti na…
Hasira; Chanzo Kikubwa cha Kuvunjika Uhusiano!
LAITI kama kwenye dunia hii kila mmoja angejitambua, akafuata misingi sahihi ya uhusiano, basi kusingekuwa na ugomvi. Watu wangekuwa wanapishana tu kwenye mambo madogomadogo na kuwekana sawa kisha maisha yanaendelea, lakini kutokana na…
Utajuaje Kama Umempata Mtu Sahihi? Soma Hapa
YAWEZEKANA kwa kipindi kirefu ulikuwa ukitamani kumpata mpenzi wa kweli ambaye atakupenda na kukufanya uyafurahie mapenzi na maisha kwa jumla. Mara nyingi, kila mtu huwa na matarajio yake ndani ya kichwa chake.
Kinachowakwamisha…
Faida Za Wapendanao Kuwa Marafiki
UTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.
Mwanaume…
Kusikilizana; Silaha Kubwa Ya Kudumisha Penzi
NI siku nyingine Mungu ametupa pumzi tunaendelea kusukuma gurudumu la maisha yetu ya hapa duniani, yatupasa tumrudishie yeye sifa na utukufu. Kwa wale wenye changamoto mbalimbali kama za magonjwa, tunawaombea wapone haraka! Nikirudi…
Sifa 5 Za Mwanamke Ambaye Ni ‘Wife Material’
WIKI hii nitazungumzia sifa tano za mwanamke ambaye anastahili kuwa mke au kwa kizungu tunasema ‘wife material’. Nafanya hivi ikiwa ni msaada kwa wale ambao wamefikia hatua ya kuingia kwenye ndoa lakini bado wanashindwa kutambua yupi ni…
Aina 10 Za Wanawake Wanaopendwa Na Wanaume
KARIBU jamvini mdau, ni siku nyingine tunakutana tena hapa kupeana elimu ya uhusiano wa kimapenzi na maisha kwa jumla. Nimekwishaeleza mara kadhaa kwamba wote tumezaliwa tukiwa safi kabisa. Mambo mengine hujitokeza huko katikati kadiri…
Ukisikiliza wanasema nini juu yako, huwezi kufanikiwa kamwe!
Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima na unaendelea kupambana kuhakikisha maisha yako yanakuwa mazuri.
Mimi namshukuru Mungu kwa kuwa amenipa afya njema na maarifa ambayo nayatumia katika…
Usimuache kwa udhaifu wake, utampata wapi mkamilifu?
WATU wengi ambao wana matatizo katika ndoa au uhusiano wao wa kimapenzi, wanapokuja kwangu kwa lengo la kutaka ushauri, huwa nina desturi ya kuwapa kwanza nafasi ya kujieleza kwa uhuru na uwazi tena katika mazingira tulivu. …
Kuna Wakati Penzi Linakufa Jiandae Kwa Maamuzi Magumu!
KUNA wakati unafika, moyo huwa unakinahi. Hautaki tena kusikia kitu kinachoitwa mapenzi, hicho ni kipindi ambacho kinasababisha maumivu makubwa kwa wapendanao.
Mapenzi ni hisia. Unapokuwa umempenda mtu, ukawa na malengo naye halafu…
Ukiwa Kwenye Ndoa, Mazoea Na Watu Wa Nje Ni Sumu Hatari
“MIMI nipo kwenye ndoa, huu ni mwaka wa tatu sasa. Tatizo lililonifanya niombe ushauri, mume wangu ana kawaida ya kuwa anachati na wafanyakazi wenzake wa jinsia ya kike kwenye simu yake, na wakati mwingine hata mbele yangu. “Nimegombana…
Jinsi Ya Kumpata Mwenza Katika Dunia Iliyojaa Wajeruhiwa
ULIMWENGU wa sasa, wapendanao wengi wanaishi kwa machale. Ni staili ile ya mguu pande, mguu sawa. Kwamba ukimzingua, anakuzingua. Mwaga mboga amwage ugali. Hataki kuona inakula kwake kama vijana wa sasa wanavyosema.
Kila mtu…
Ifahamu figo yako inavyoweza kuharibika
LEO tutakuelimisha kuhusu chanzo cha maradhi ya figo na tutakueleza dalili zake ili ufahamu jinsi ya kujikinga. Figo ni sehemu ya kiungo cha mwilini (ogani) inayoshirikiana na moyo, kuathirika kwake kuna athari kubwa kwa mfumo wa damu na…
Amekuvunja Moyo Wako Na Kukuacha Na Majonzi Soma Hapa
MAUMIVU katika mapenzi huwa hayazoeleki. Hata kama unajifanya wewe ni shujaa kiasi gani, inapotokea yule unayempendaye akakuumiza, akauvunja moyo wako, akaondoka na kwenda mbali na wewe, lazima utaumia sana!
Maumivu ya kimapenzi…